Simba yapania kunogesha rekodi ya Kimataifa Jumapili

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Dec 2018
Simba yapania kunogesha rekodi ya Kimataifa Jumapili
Uzuri wa rekodi ya Simba katika michuano ya Kimataifa unajieleza wenyewe.

Hakuna ubishi, unapozungumzia rekodi nzuri kwenye michuano ya Afrika kwa timu za Tanzania, jina la Simba litakuwa nafasi ya juu kabisa.

Simba ndiyo klabu pekee Tanzania iliyofika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika, mwaka 1974 ikiitoa timu ngumu ya Ghana katika Robo Fainali, Hearts Of Oak kwa jumla ya mabao 2-0.

Simba pia ni klabu pekee ya Tanzania, iliyocheza fainali ya michuano ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Hiyo ilikuwa ni mwaka 1993, ilipofanikiwa kutinga fainali ya Kombe la CAF, (sasa limeunganishwa na Kombe la Washindi na kuwa Kombe la Shirikisho) na kufungwa na Stella ya mjini Abidjan, Ivory Coast.

Bahati haikuwa yao Wekundu wa Msimbazi, kwani baada ya kulazimisha sare ya bila kufungana ugenini, walipoteza mchezo wa nyumbani kufungwa 2-0

Klabu hiyo pia ilifanikiwa kuwa ya pili Tanzania kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2003, baada ya Yanga kuwa ya kwanza mwaka 1998.

Lakini Simba ilitinga hatua hiyo kibabe zaidi, ikiwatoa waliokuwa mabingwa watetezi, Zamalek ya Misri, kwa mikwaju ya penati.

Hiyo ilifuatia ushindi wa 1-0 mjini Dar es Salaam, kabla ya kwenda kufungwa 1-0 na yenyewe pia Cairo, lakini mchezo ulipohamia kwenye mikwaju ya penalti, Juma Kaseja, mtaalamu wa kuokoa michomo hiyo, aliibeba Simba baada ya kucheza penalti mbili.

Baada ya kukosekana kwa miaka mitano kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Afrika, hatimaye timu yenye rekodi nzuri zaidi nchini kwenye michuano hiyo, Simba SC imerejea mwaka huu baada ya mwaka jana kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho.

Simba ilianza michuano hiyo kwa kishindo baada ya kuifumua Mbabane Swallows jumla ya mabao 8-1 katika michezo yote miwili ya hatua ya awali iliyopigwa Tanzania na kule eSwatini Simba ikifunga mabao manne katika kila mchezo.

Katika raundi ya kwanza ya michuano hiyo, ilianza kwa kufungwa mabao 2-1 na Nkana Fc katika mchezo uliopigwa nchini Zambia wiki iliyopita

Lakini keshokutwa Jumapili, ikicheza katika dimba lake la nyumbani Simba itakuwa na nafasi ya kupindua matokeo na kuweza kutinga hatua ya makundi kwa mara ya pili katika historia yake baada ya kufanya hivyo mwaka 2003.

Simba inahitaji ushindi wa bao 1-0 tu ili ijihakikishie nafasi kuwa miongoni mwa timu 16 bora barani Afrika.

Jambo hilo linawezekana, rekodi ya Simba dhidi ya Nkana kwenye michezo ya nyumbani inajieleza.

Katika michezo miwili ambayo Nkana imekuja kucheza na Simba hapa Tanzania, imefungwa jumla ya mabao matano huku yenyewe ikishindwa kufunga bao hata moja ingawa katika michezo yote timu hiyo ilifanikiwa kutinga hatua inayofuata kutokana na ushindi mnono iliyopata nyumbani

Ushindi dhidi ya Nkana keshokutwa utan'garisha zaidi rekodi ya Simba kwenye michuano ya Kimataifa.

Lakini pia ushindi utaitajirisha zaidi Simba kwani itakuwa na uhakika wa kuvuna zaidi ya Bil 1.2 kwa kufanikiwa kutinga hatua hiyo
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
27m ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
15h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
16h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
19h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’