Jumapili Simba itakuwa na kibarua cha kusaka nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika itakapochuana na Nkana Fc.
Simba inahitaji ushindi wa angalau bao 1-0 ili iweze kutinga hatua ya makundi.
Mashabiki wa Simba na Watanzania wote kwa ujumla wamehamasishwa kujitokeza kwa wingi dimba la Taifa siku hiyo ili kuipa sapoti Simba ambayo itakuwa ikipeperusha bendera ya nchi.
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems ni miongoni mwa waliowaasa mashabiki kujitokeza kwa wingi kuujaza uwanja wa Taifa kuiunga mkono Simba
Kwani mafanikio ya Simba katika mchezo huo yatachangia mafanikio ya soka la Tanzania.
Wengi wamekuwa wakijiuliza kwa nini baadhi ya nchi zinatoa hadi timu nne katika michuano ya vilabu barani Afrika wakati Tanzania tuna nafasi mbili tu?
Ukweli ni kwamba idadi ya timu inachangiwa na mafanikio ya nchi husika katika michuano iliyopita.
Nchi inapoingiza timu katika hatua ya makundi kuna alama inapewa na CAF.
Alama hizo huongezeka kadiri timu inapofanya vizuri kuanzia hatua hiyo ya makundi mpaka kuchukua ubingwa

Hivyo kama Simba itafanya vizuri itakuwa faida kwa nchi kwani baadae CAF itaweza kuiongezea Tanzania timu za kushiriki michuano yake ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho kama itafikisha alama zinazohitajika.

ADVERTISE HERE