Mburkinabe Zana Coulibaly leo ameanza kuitumikia Simba kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara ikiwa ni takribani wiki tatu zimepita tangu ajiunge na mabingwa hao wa Tanzania Bara.
Katika mchezo huo ambao Simba imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMC, Coulibaly ameonyesha kiwango kizuri.
Yuko makini kwenye kukaba na ameonyesha uwezo wa kupiga pasi za uhakika na krosi
Bao la kwanza la Simba lililofungwa na Adam Salamba yalikuwa ni matokeo ya majaro yake aliyomimina kutoka upande wa kulia kabla ya mpira huo kuwahiwa na Niyonzima aliyemtengea Salamba krosi iliyozaa bao
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesifu kiwango kilichoonyeshwa na beki huyo na amesema atakuwa bora zaidi kadiri atakavyokuwa akicheza na kuzoeana na wenzie
Aussems amewapongeza wachezaji wake kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi huo ingawa amesema hawakucheza vizuri kwenye dakika 30 za mwisho

ADVERTISE HERE