Murshid apigiwa 'chapuo' arejeshwe kikosini Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Dec 2018
Murshid apigiwa 'chapuo' arejeshwe kikosini Simba
Mlinzi wa Kimataifa wa Simba Juuko Murshidi huenda akajumuishwa katika kikosi cha timu hiyo kitakachoikabili Nkana Fc kwenye mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa siku ya Jumapili

Makosa yaliyofanywa na safu ya ulinzi katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Zambia, yanatajwa kuigharimu Simba kupoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 2-1

Murshid ambaye ana uzoefu wa michezo ya Kimataifa, amependekezwa arejeshwe kikosini kuchukua nafasi ya mkongwe Paschal Wawa ambaye hakuwa na mchezo mzuri nchini Zambia

Beki huyo wa kutumainiwa wa timu ya Taifa ya Uganda pia anaweza kucheza sambamba na Wawa kama kiraka Erasto Nyoni atahamishwa kucheza namba mbili.

Juuko aliondolewa katika kikosi kilichosafiri kwenda Zambia na kocha Patrick Aussems baada ya kuchelewa kujiunga na kambi ya Simba iliyokuwa ikijiwinda na mchezo huo.

Licha ya ubora wake, mara kwa mara Murshid amekuwa akiingia katika mgogoro na makocha na viongozi wa Simba kutokana na tabia yake ya kutofuata maelekezo anayopewa

Murshid amekuwa na kawaida ya kuchelewa kuripoti kambini kila anapokwenda kuitumikia timu ya Taifa ya Uganda.

Pierre Lechantre ambaye aliinoa Simba kabla ya kutua Aussems, aliwahi kumuondoa kabisa kikosini akimtuhumu mchezaji huyo kuwa 'mtukutu'

Aussems alipendekeza Murshid arudishwe kikosini baada ya kumuona akifanya vizuri na timu ya Taifa ya Uganda ambayo tayari imekata tiketi ya kutinga fainali za michuano ya AFCON 2019

Hata hivyo aliamua kumuondoa katika kikosi kilichokwenda Zambia baada ya kuchelewa kuripoti kambini
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’