Makocha wazalendo wampa Aussems mbinu za kuimaliza Nkana FC

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
โ€ข
18 Dec 2018
Makocha wazalendo wampa Aussems mbinu za kuimaliza Nkana FC
Wakufunzi mbalimbali wa soka nchini wametoa maoni yao juu ya nini kifanyike ili kuiwezesha Simba kuichapa Nkana Fc na kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Mmoja wa wataalam hao Kennedy Mwaisabula amesema mchezo huo wa marudiano hautakuwa mwepesi kama wengi wanavyodhani kwani hata Nkana inasaka nafasi ya kutinga hatua ya makundi huku ikiwa tayari iko mbele kwa mabao 2-1, ushindi iliyopata katika mchezo wa kwanza.

Lakini Mwaisabula amesema kama Aussems atabadili mfumo wake ikiwa ni pamoja na kumpumzisha Paschal Wawa na kumtumia Juuko Murshid beki ya kati, Simba inaweza ikafanikiwa

Mtaalamu huyo amesema kwenye mchezo huo wa nyumbani, Aussems anapaswa kutumia viungo watano tofauti na alivyowatumia watatu Chama, James Kotei na Jonas Mkude katika mchezo wa kwanza na kupelekea timu kuzidiwa sehemu ya kiungo.

โ€œChama asingeweza kufanya vizuri mechi hiyo maana alikuwa anacheza na watu wanaomfahamu vizuri, mbaya zaidi kocha aliweka viungo wachache ndiyo maana walibanwa sana katikati kuliko wenzao waliokuwa wanafunguka zaidi, Mwaisabula amenukuliwa na Mwanaspoti"

โ€œKingine Simba hawapaswi kukaa na matumaini ya kubebwa na faida ya goli la ugenini, huko ni kujipoteza na kujiondoa kwenye mstari, bali wanatakiwa kufanya maandalizi kwa kuweka mawazo kuwa walipoteza mechi ya kwanza,โ€ alisema.

Naye Dk Mshindo Msolla amesema;

โ€œNi kweli wamepata faida ya bao la ugenini lakini Nkana ni timu inayonekana kuwa na uwezo wa kushinda hata ugenini, waliifunga UD Songo kwao Msumbiji.

"Muhimu pia ni namna ambavyo kocha atafanyia kazi kasoro za mchezo uliopita. Anatakiwa ashambulie zaidi kwenye mechi ya nyumbani.

โ€œKwa mfano Chama alishindwa kufurukuta kama matarajio ya wengi kwasababu alikutana na wachezaji wanaomfahamu kuliko hata wenzake wa Simba, ilikuwa ni lazima mechi hiyo apate tabu sana, ila wana nafasi ya kusonga mbele endapo tu watajitambua na kocha atafanyia kazi mapungufu,โ€ alisema Dk Msolla.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE โ†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE โ†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE โ†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE โ†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE โ†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE โ†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE โ†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE โ†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE โ†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE โ†’