Uongozi wa klabu ya Simba umeweka hadharani viingilio vya mchezo wa marudio wa ligi ya mabingwa kati ya Simba dhidi ya Nkana Fc utakaopigwa Jumapili ijayo, Disemba 23 kwenye uwanja wa Taifa.
Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema kiingilio cha chini kabisa kuweza kuushuhudia mchezo huo ni Tsh 3,000/- tu lengo likiwa kuwapa nafasi Watanzania na mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa ili kuwaunga mkono mabingwa hao wa Tanzania wanaosaka tiketi muhimu ya kutinga hatua ya makundi.
Kwa majukwaa ya VIP viingilio vitakuwa Tsh 20,000/- kwa VIP A na Tsh 10,000/- kwa VIP B
"Njooni siku ya Jumapili kwa wingi Taifa tuvae jezi zetu nyeupe na nyekundu kuishangilia timu yetu iweze kupata ushindi tufuzu tuende hatua ya makundi, Vigoma vyote vya amsha amsha vitakuwepo," amesema Manara

Simba inahitaji ushindi wa angalau bao 1-0 ili kutinga hatua ya makundi na kujihakikishia zawadi ya kitita cha Tsh Bilioni moja kwa kutinga hatua hiyo.

ADVERTISE HERE