Uongozi wa klabu ya Simba leo unatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari kuelezea mikakati yake kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Nkana Fc.
Mchezo huo wa marudiano utapigwa Jumapili ijayo, Disemba 23 kwenye uwanja wa Taifa.
Simba ina nafasi adimu ya kutinga hatua ya makundi kama itaibuka na ushindi kwenye mchezo huo ikihitaji kushinda hata bao 1-0.
Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema katika Mkutano huo atatangaza viingilio vya mchezo huo ambapo amebainisha kuwa wameamua kuvipunguza ili kuwapa nafasi mashabiki wengi kufurika uwanja wa Taifa kuiunga mkono Simba.
"Hii ni nafasi muhimu sana kwa Simba kutinga hatua ya makundi," amesema Manara
"Tumeanzisha kampeni ya kufa na kupona ili kuwahamasisha Watanzania wote waje uwanjani. Kama Simba itatinga hatua ya makundi ni mafanikio kwa Tanzania."
"Ikumbukwe hatujashiriki hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa kwa miaka 15. Mara ya mwisho kwa timu ya Tanzania kutinga hatua hiyo ilikuwa mwaka 2003," amesema

ADVERTISE HERE