Aussems kufanya mabadiliko ya kikosi mchezo dhidi ya KMC

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Dec 2018
Aussems kufanya mabadiliko ya kikosi mchezo dhidi ya KMC
Licha ya kukabiliwa na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya KMC kesho Jumatano, mawazo yote ya Wana Msimbazi ni kwenye mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa dhidi ya Nkana Fc utakaopigwa Jumapili katika dimba la Taifa.

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema wanahitaji kushinda mchezo wa kesho ili kuweka juu morali ya wachezaji wake kuelekea mchezo huo wa Jumapili.

Aussems amesema atafanya mabadiliko kidogo ya kikosi chake katika mchezo huo utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa kuanzia saa 12 jioni.

Simba inahitaji kushinda michezo yake yote ya kiporo ili kuzifikia Yanga na Azam ambazo zimeshashuka dimbani mara 16 wakati mabingwa hao watetezi wakiwa wamecheza michezo 12 tu.

Simba ina deni la alama 17 dhidi ya Yanga na alama 13 dhidi ya Azam FC hivyo kufanya ushindi kuwa matokeo ya lazima kwenye michezo yote ya viporo.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’