FT : Prisons 0-1 Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Nov 2017
FT : Prisons 0-1 Simba
Wekundu wa Msimbazi, Simba leo wametimiza ahadi ya kuondoka na alama zote sita mkoani Mbeya baada ya kuilaza Prisons bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa kwenye dimba la Sokoine.

Kikosi cha Prisons kilionyesha upinzani wa hali ya juu leo lakini shukrani za pekee zimuendee mkongwe John Bocco 'Adebayor' aliyepachika bao la Simba kwenye dakika ya 83.

Ushindi huu umefuta rekodi mbaya ya Simba kwenye uwanja wa Sokoine ambapo tangu mwaka 2014 Simba ilikuwa haijaondoka na ushindi kwenye dimba hilo.

Matokeo hayo pia yanaihakikishia Simba kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kukamilika mzunguuko wa 10.

Imefikisha alama 22, alama ambazo zinaweza kufikiwa na Azam FC pekee kama itashinda mchezo wake dhidi ya Njombe Mji.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
4h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
10h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
13h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’