Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema maandalizi kuelekea mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Nkana Fc yameanza kwa kuzindua operesheni ya KUFA NA KUPONA
Operesheni hiyo ni maalum kwa ajili ya kuwashawishi mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Taifa katika huo utakaopigwa Jumapili ijayo, Disemba 23 2018

Kesho Jumanne Manara ataweka wazi viingilio vya mchezo huo ambao Simba inahitaji ushindi wa bao 1-0 tu ili iweze kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo namba moja kwa ukubwa barani Afrika katika ngazi ya vilabu
Manara amesema mashabiki wajiandae kufurika uwanja wa Taifa kwani wanakusudia kupunguza gharama za viingilio lengo likiwa ni kuhakikisha mashabiki wa Simba na Watanzania wazalendo kwa wingi wao wanamudu ili kuujaza uwanja wa Taifa unaochukua mashabiki takribani elfu 60

ADVERTISE HERE