Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kitaondoka nchini Zambia leo kurudi Tanzania baada ya kukamilisha mchezo wa kwanza wa michuano ya ligi ya mabingwa dhidi ya Nkana Fc.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na uongozi wa timu hiyo, Simba itaondoka Zambia saa nane mchana siku ya leo Jumapili, Disemba 16 2018 na itawasili Tanzania kesho saa 9:40 usiku
Jana mabingwa hao wa nchi walifanikiwa kupata bao la ugenini katika mchezo ambao Nkana ilishinda kwa mabao 2-1
Matokeo hayo yameweka hai matumaini ya Simba kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo sasa ikihitaji ushindi wa angalau bao 1-0 katika mchezo wa marudiano utakaopigwa uwanja wa Taifa Jumapili ijayo, Disemba 23 2018.

ADVERTISE HERE