Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema licha ya kufungwa mabao 2-1 na Nkana Fc katika mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa jana, bado wana nafasi ya kutinga hatua ya makundi kama watashinda mchezo wa marudiano utakaopigwa kwenye dimba la Taifa Jumapili ijayo.
Aussems amesema timu yake haikucheza vizuri hasa katika kipindi cha kwanza, waliwapa wapinzani wao nafasi ya kumiliki mpira.
Amesema Nkana ni timu nzuri, walistahili ushindi waliopata kwenye uwanja wao wa nyumbani jana kwa kuwa walicheza vizuri.
Hata hivyo mchezo bado haujamalizika na Simba pia itakuwa na nafasi ya kutumia vyema uwanja wake wa nyumbani wiki ijayo
"Tunakwenda kujipanga, kama wao wameshinda kwao basi na sisi tunaweza kupata ushindi kwetu na tutasonga mbele," alisema Aussems baada ya mchezo jana.
Baadhi ya wadau wamekosoa mpango alioingia nao Aussems kwenye mchezo wa jana kwa kutumia washambuliaji watatu ikitajwa kuwa moja ya sababu iliyowapa Nkana nafasi ya kutawala safu ya kiungo.
"Kwa jinsi mchezo ulivyokuwa sikuona kama kulikuwa na ulazima wa kocha kupanga washambuliaji watatu," amesema Rashid mdau kutoka jijini Mwanza.
"Tungeweza kuwa na mshambuliaji mmoja halafu hizi nafasi mbili tungeweka viungo Dilunga na Kichuya ambao wangesaidiana na kina Chama, Mkude na Kotei katika safu ya kiungo"
"Lakini pia kocha wetu asiwe mzito kwenye kufanya mabadiliko. Ni vyema mchezaji anapokuwa ametoka mchezoni akapumzishwa. Kuchelewa kufanya mabadiliko kunaigharimu Simba mara kwa mara"
"Hawa NKana ni wa kawaida sana, tunao uwezo wa kuwafunga goli nyingi tu kwenye uwanja wa Taifa. Muhimu kocha afanyie kazi mapungufu yaliyojitokeza hasa kwenye safu ya ulinzi"
Kikosi cha mabingwa hao wa Tanzania Bara kinarejea leo usiku kutoka nchini Zambia ambapo uongozi umesema wataanza maandalizi ya mchezo wa marudiano mara moja.
Simba itahitaji ushindi wa bao 1-0 tu kwenye mchezo wa marudiano ili iweze kutinga hatua ya makundi.

ADVERTISE HERE