Afisa Habari wa Simba Haji Manara amewataka mashabiki kujiandaa kufurika kwa wingi kwenye mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa dhidi ya Nkana Fc utakaopigwa wiki ijayo.
Manara amesema licha ya Simba kupoteza mchezo wa leo, ina nafasi ya kutinga hatua ya makundi kama itashinda kwa bao 1-0 katika mchezo huo wa marudiano.
Sasa kuhakikisha timu inapata sapoti ya kutosha kutoka kwa mashabiki katika mchezo huo, kampeni maalum ya kuwashawishi mashabiki itakayofahamika kwa jina la OPERESHENI KUFA NA KUPONA itazinduliwa Jumatatu
Kikosi cha Simba kinatarajiwa kurejea nchini kesho saa tisa usiku kuanza maandalizi ya mchezo huo wa marudiano utakaopigwa uwanja wa Taifa Disemba 23 2018

ADVERTISE HERE