Dirisha dogo la usajili lililofunguliwa Novemba 15 2018 litafungwa leo Jumamosi Disemba 15, saa 5:59 usiku.
Katika taarifa yake iliyotolewa mapema wiki hii, TFF imevitaka vilabu kutuma orodha ya wachezaji waliowaongeza katika usajili huu wa dirisha dogo.
Aidha, TFF imefafanua kuwa timu inaweza kuongeza idadi ya wachezaji kama haikusajili wachezaji 30 wakati wa kipindi cha usajili wa dirisha kubwa.
Pia Klabu ikimtoa mchezaji kwa mkopo haitoi nafasi ya kusajili mchezaji mwingine,mchezaji aliyetolewa kwa mkopo bado ni mchezaji wa klabu husika.
Usajili huu wa dirisha dogo umekusudia kujaza nafasi za wachezaji kama hawakutimia 30 wakati wa kipindi cha usajili wa dirisha kubwa na kwa wale waliomaliza mkataba na klabu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Simba Crenstencias Magori amesema Simba haitasajili mchezaji mwingine baada ya kukamilisha usajili wa mlinzi wa kulia, Zana Coulibaly
Magori ambaye yuko nchini Zambia na kikosi cha Simba ambacho leo kinashuka dimbani kuikabili Nkana Fc kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa, amesema timu hiyo imeachana na mpango wa kusajili mchezaji mwingine kutokana na ufinyu wa muda.
"Nadhani tuna kikosi imara kitakachoweza kufanya vizuri msimu huu," amesema Magori
"Awali tulikuwa na mpango wa kusajili mchezaji mwingine kuongeza nguvu kwenye safu yetu ya usambuliaji lakini tumeachana na mpango huo"
Aidha Magori amesema Simba imegoma kuwauza nyota wake Meddie Kagere na Emmanuel Okwi waliokuwa wakiwaniwa na timu za AS Vital Club na Kaizer Chiefs.
Coulibaly amesajiliwa kuziba nafasi ya Shomari Kapombe ambaye amepata majeraha ambao huenda yakamuweka nje kwa muda mrefu.
Simba imemtoa kwa mkpo Mohammed Rashid kwenda KMC huku mlinda lango Said Mohammed 'Nduda' nae ikielezwa yuko mbioni kukamilisha uhamisho wake wa mkopo kwenda klabu ya Ndanda Fc

ADVERTISE HERE