Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema mchezo wa kesho wa ligi ya mabingwa dhidi ya Nkana Fc unaopigwa nchini Zambia hautakuwa mwepesi
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari akielezea maandalizi ya mchezo huo, Aussems amesema ameifuatilia Nkana Fc na amebaini ina safu nzuri ya ulinzi na pia wako vizuri katika ushambuliaji
Hata hivyo Aussems amesema ameiandaa timu yake kikamilifu kuhakikisha wanapata matokeo mazuri watakayorudi nayo jijini Dar es salaam kuelekea mchezo wa marudiano.
"Tunafahamu mchezo hautakuwa mwepesi. Tumefuatilia Nkana tumebaini wana kipa mzuri, walinzi wazuri wa kati. Kwa ujumla safu yao ya ulinzi ni nzuri," amesema
"Pia safu yao ya ushambuliaji ni nzuri wakiwa na wachezaji kama Bwalya, Chisala, Ngulumbe, Kampamba, wana wachezaji wazuri"
"Tunafahamu, tunaanzia ugenini hivyo tunapaswa kuwa makini. Kila timu ina nafasi kwa asilimia 50 ya kupata matokeo katika michezo yote miwili. Ingawa kwa mchezo wa kesho wenzetu watakuwa nyumbani," amesema
Nae Haruna Niyonzima amesema morali ya wachezaji iko juu na wako tayari kwa mchezo huo.
Wanafahamu mchezo hautakuwa rahisi kwa sababu wako ugenini lakini wamejiandaa kikamilifu kupata matokeo

ADVERTISE HERE