Simba iko tayari kwa 'mtanange' wa kesho

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Dec 2018
Simba iko tayari kwa 'mtanange' wa kesho
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema vijana wake wako tayari kwa ajili ya mchezo wa raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa dhidi ya Nkana Fc.

Mchezo huo utapigwa kesho Jumamosi, Disemba 15 saa kumi kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki katika dimba la Nkana, Kitwe Zambia

Aussems amesema anafahamu Nkana watakuwa katika presha ya kupata ushindi nyumbani na watacheza mchezo wa kushambulia lakini nao 'hawatapaki basi', watashambulia pia

"Hatutacheza kwa kujilinda muda wote, hilo litakuwa kosa kwetu na wapinzani wetu wanaweza wakatuadhibu, tutapambana dakika zote na tutacheza soka la kushambulia kujaribu kuwapa presha,” alisema Aussems.

β€œTunajua Nkana wanauzoefu na mashindano ya kimataifa, lakini tunataka kujaribu kurahisisha mchezo wa marudiano kwa kujaribu kupata ushindi kwenye mchezo wa hapa”

Kikosi cha Simba kimejifua nchini Zambia kwa siku mbili tangu kilipowasili juzi mchana.

Leo Simba itafanya mazoezi kwenye uwanja wa Nkana unaochukua takribani mashabiki 10,000.

Uwanja huo utatumika kwenye mchezo wa kesho unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini Zambia na hapa Tanzania
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18m ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
14h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
18h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’