Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema vijana wake wako tayari kwa ajili ya mchezo wa raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa dhidi ya Nkana Fc.
Mchezo huo utapigwa kesho Jumamosi, Disemba 15 saa kumi kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki katika dimba la Nkana, Kitwe Zambia
Aussems amesema anafahamu Nkana watakuwa katika presha ya kupata ushindi nyumbani na watacheza mchezo wa kushambulia lakini nao 'hawatapaki basi', watashambulia pia
"Hatutacheza kwa kujilinda muda wote, hilo litakuwa kosa kwetu na wapinzani wetu wanaweza wakatuadhibu, tutapambana dakika zote na tutacheza soka la kushambulia kujaribu kuwapa presha,β alisema Aussems.
βTunajua Nkana wanauzoefu na mashindano ya kimataifa, lakini tunataka kujaribu kurahisisha mchezo wa marudiano kwa kujaribu kupata ushindi kwenye mchezo wa hapaβ
Kikosi cha Simba kimejifua nchini Zambia kwa siku mbili tangu kilipowasili juzi mchana.
Leo Simba itafanya mazoezi kwenye uwanja wa Nkana unaochukua takribani mashabiki 10,000.
Uwanja huo utatumika kwenye mchezo wa kesho unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini Zambia na hapa Tanzania

ADVERTISE HERE