Kiungo Clatous Chama ni mchezaji maarufu sana nchini Zambia.
Uwepo wake kwenye kikosi cha Simba umewafanya Wazambia wengi kuusubiri kwa hamu mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Nkana Fc.
Licha ya kuwa ugenini, huenda Simba ikapata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa Wazambia wanaovutiwa na Chama ambaye pia ni mmoja wa wachezaji wanaounda kikosi cha timu ya Taifa ya Zambia 'Chipolopolo'
Msemaji wa Simba Haji Manara jana alipokutana na Meneja wa Power Dyamos iliyoipa Simba uwanja wa kufanyia mazoezi kuelekea mchezo huo, amefichua kuwa Meneja huyo alimwambia kuwa sehemu ya video wakati akimtambulisha Chama siku ya Tamasha la SIMBA DAY imekuwa maarufu sana nchini Zambia

Mashabiki wengi nchini humo wamekuwa na shauku ya kuiona Simba ikiwa na kiungo huyo aliyejitengenezea heshima nchini Zambia na hapa Tanzania
Mchezo baina ya timu hizo utapigwa keshokutwa Jumamosi Disemba 15 2018 katika jiji la Kitwe, ambako ndipo ulipo uwanja wa Nkana Fc.

ADVERTISE HERE