Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wako nchini Zambia ambapo keshokutwa Jumamosi wanashuka katika dimba la Nkana huko Kitwe kuwakabili wenyeji wao Nkana Fc katika mchezo wa raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
Hii itakuwa mara ya tatu kwa Simba kushuka katika dimba hilo katika michuano ya Afrika ikipoteza michezo yote iliyocheza nchini humo
Mara ya kwanza mwaka 1994 Simba ililala kwa mabao 4-1 kabla ya kulipa kisasi kwenye dimba la Taifa (Uwanja wa Uhuru) kwa ushindi wa mabao 2-0
Awamu ya pili Simba ikafungwa tena 4-0 katika uwanja huohuo na yenyewe kushinda kwa mabao 3-0 kwenye mchezo wa marudiano.
Kocha wa mabingwa hao wa nchi Patrick Aussems amekwenda Zambia akiifahamu rekodi hiyo na ameahidi kuwaduwaza Wazambia hao katika ardhi yao.
"Rekodi zinaonyesha hatujawahi kuifunga Nkana kwenye ardhi yao lakini kwangu sio tatizo kwa kuwa rekodi hazichezi mpira," amesema Aussems.
"Nimeiandaa timu yangu kikamilifu kuhakikisha tunapata matokeo mazuri yatakayokuwa na faida kwetu kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa jijini Dar es salaam wiki ijayo"
Simba ilitua Zambia jana mchana na jioni kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Dynamos unaomilikiwa na klabu ya Power Dynamos timu aliyokuwa akiichezea Cleotus Chama kabla ya kusajiliwa na Simba mwanzoni mwa msimu huu

ADVERTISE HERE