Tathmini mchezo wa Prisons v Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Nov 2017
Tathmini mchezo wa Prisons v Simba
Baada ya kupumzika kwa wiki mbili kikosi cha Simba, leo kinashuka uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya kuwakabili Maafande wa Tanzania Prisons katika mchezo wa mzunguko wa 10 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Simba itaingia kwenye mchezo huo ikiwa ndiyo vinara wa ligi kwa kujikusanyia pointi 19, katika michezo tisa waliyocheza huku Tanzania Prisons wakiwa kwenye nafasi ya tano kwenye msimamo wakiwa na pointi 14.

Mechi ya mwisho Simba ilicheza kwenye uwanja huo wa Sokoine dhidi ya wenyeji wengine Mbeya City, na kushinda bao 1-0, bao ambalo limelalamikiwa na wenyeji Mbeya City wakidai mfungaji Shiza Kichuya alikuwa amezidi, lakini Tanzania Prisons wao mechi ya mwisho walipata sare ya ugenini kwenye uwanja wa Kaitaba Bukoba, baada ya kwenda nao sare ya kufungana 1-1.

Matokeo hayo yanaufanya mchezo huo kuwa mgumu na wenye ushindani wa aina yake kwani kila upande umejidhatiti kuhakikisha unapata pointi tatu na kuendelea kujiweka sawa kwenye msimamo wa ligi hiyo ambayo imeonekana kuwa ngumu na ushindani mkubwa msimu huu.

Simba mbali na kupewa nafasi kubwa ya ushindi kutokana na ubora wa kikosi chake lakini itawabidi kucheza kwa tahadhari kubwa kwani msimu uliopita waliweza kuacha pointi tatu kwenye uwanja huo mbele ya Maafande hao mabao ya mshambuliaji Peter Hangaya, ambaye alimtungua kipa Mu Ivory Coast Vicent Angban na Simba kupoteza mchezo kwa mabao 2-1.

Uwepo wa mshambuliaji anayewaniwa na Yanga Mohamed Rashid mwenye mabao sita kwenye kikosi cha Prisons, kunawapasa Simba kucheza kwa tahadhari kwani vinginevyo wanaweza kujikuta wanapoteza mchezo huo kwamara ya kwanza msimu huu na kuwapa mwanya wapinzani wao Yanga kuongoza ligi endapo watashinda mchezo wao wa Jumapili dhidi ya Mbeya City.

Simba inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kikosi kamili kisicho na majeruhi lakini ikiwategemea zaidi washambuliaji wake Emmanuel Okwi na John Bocco wakati kwenye eneo la kiungo Haruna Niyonzima na Jonas Mkude wakitarajiwa kuzuia na kuanzisha mashambulizi ya timu hiyo .

Kocha Joseph Omog, ataendelea kutumia mfumo wake wa 4-4-2, ambao siku zote amekuwa akiuheshimu na kumpa matokeo hasa anapotafuta pointi tatu.

Kwaupande wao Tanzania Prisons wameapa kuhakikisha wanakuwa timu ya kwanza kuifunga Simba,na kupunguza gepu la pointi kutoka tano hadi mbili.

Silaha kubwa ya Maafande hao ni rekodi nzuri waliyokuwa nayo dhidi ya timu hiyo ambayo imekuwa ikiwasumbua sana kila wanapokutana nao kwenye uwanja wowote ule hata ule wa Uhuru Dar es Salaam.

Rashid ndiyo tegemezi kubwa la Tanzania Prisins, katika safu ya ushambuliaji na bila shaka atawekwa mstari wa mbele, kwa matarajio ataendeleza rekodi yake ambayo ameanza nayo msimu huu katika ufungaji.

Simba inahitaji kucheza kufa na kupona kupata ushindi ili kuendelea kuongoza ligi vinginevyo inaweza kupoteza mwelekeo na kujikuta inavurugikiwa mipango yake ya kutwaa ubingwa msimu huu.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
4h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
10h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
13h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’