Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kiko katika ardhi ya Zambia kikiendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Nkana Fc utakaopigwa Jumamosi Disemba 15.
Baada ya kuwasili nchini Zambia mapema leo, jioni Simba ilijifua katika uwanja wa Dynamos unaomilikwa na klabu ya Power Dynamos inayoshiriki ligi kuu ya Zambia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Simba Crescentius Magori aliyeongoza msafara wa viongozi wa timu hiyo, walipata nafasi ya kujadiliana masuala kadhaa na wenzao wa Dynamos kuelekea mchezo huo wa Jumamosi
Viongozi wengine walio katika msafara huo ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Dk Zawadi Kadunda na Afisa Habari wa Simba Haji Manara

ADVERTISE HERE