Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amefichua kuwa beki wake mpya Zana Coulibaly huenda akaanzia kuitumikia timu hiyo Disemba 19 kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya KMC
Aussems amesema wanatarajia 'ITC' ya beki huyo aliyesajiliwa kutoka ASEC Mimosas itawasili mapema kabla ya mchezo huo utakaopigwa baada ya Simba kurejea kutoka Zambia.
Aidha Coulibaly hataweza kuitumikia Simba kwenye michuano ya CAF kwa kuwa usajili wa michuano hiyo tayari umefungwa na utafunguliwa kabla ya kuanza kwa hatua ya makundi.
Akizungumzia maendeleo yake, Aussems amesema Coulibaly ni mchezaji mzuri na anaamini ataisaidia Simba wakati wote ambao itamkosa Shomari Kapombe ambaye anaendelea na matibabu nchini Afrika Kusini

ADVERTISE HERE