Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kimeendelea kujifua kwenye uwanja wa Boko Veterans jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Nkana Fc.
Mchezo huo utapigwa nchini Zambia Jumamosi ijayo, Disemba 15 mabingwa hao wa nchini wakitarajiwa kuondoka Alhamisi Alfajiri kwenda Zambia
Miongoni mwa wachezaji waliohudhuria mazoezi ya jana ni beki mpya Zana Coulibaly ambaye hata hivyo bado hajaanza kuitumikia Simba akisubiri kukamilika kwa uhamisho wake wa Kimataifa (ITC)
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema anakiandaa kikosi chake kikamilifu kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye mchezo huo wa ugenini

ADVERTISE HERE