Wakongwe waitahadharisha Simba mchezo dhidi ya Nkana Fc

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
7 Dec 2018
Wakongwe waitahadharisha Simba mchezo dhidi ya Nkana Fc
Simba imetinga raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kibabe kwa kuifumua Mbabane Swallows jumla ya mabao 8-1 katika michezo miwili ya hatua ya awali.

Ushindi huo umeongeza mzuka na kujiamini kwa kikosi cha Simba ambacho kimedhamiria kutinga hatua ya makundi.

Simba itachuana na Nkana Fc ya Zambia katika raundi ya kwanza ya michuano hiyo ambapo itaanzia ugenini mjini Kitwe wiki ijayo Disemba 14 2018.

Kuelekea mchezo huo wadau na wachambuzi mbalimbali wa soka nchini wameitahadharisha Simba kuwa ni lazima ijipange sawasawa kuweza kuiondosha Nkana Fc kwani timu hiyo sio ya kubezwa.

Pia historia baina ya timu hizo inafanya mchezo baina yao kuwa na ushindani wa aina yake. Nkana ilianzishwa mwaka 1935 wakati Simba ilianzishwa mwaka 1936

Timu zote zinatumia jezi za rangi nyeupe na nyekundu.

Mwaka 1990 Nkana Fc ilitinga fainali za michuano ya ligi ya mabingwa wakati Simba ilitinga fainali za michuano ya kombe la Washindi mwaka 1993

"Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Simba na Nkana kukutana kwenye michuano mikubwa barani Afrika," amesema Ally Mayay mmoja wa wachambuzi wa soka katika runinga ya Azam

“Simba na Nkana zilishawahi kukutana miaka iliyopita. Ifahamike kuwa Nkana ilishafika fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1990, lakini pia ina wachezaji wengi kutoka nchi zilizoendelea kisoka tofauti na Simba," amesema

“Ili Simba waweze kushinda mbele ya Nkana, ni lazima wajipange upya kwa kurekebisha makosa ambayo yalijitokeza hususan kwenye safu ya ulinzi ambayo licha ya kutofungwa kwenye mechi za kwanza, lakini inahitaji maboresho kwani wangekutana na timu nzuri wasingefika walipo sasa”

Naye Kenny Mwaisabula amesema Simba inapaswa itambue kila wanaposonga mbele katika michuano hiyo ndio ugumu unaongezeka hivyo wanapaswa kujipanga.

“Simba bado ina kazi kubwa na kila wanavyosonga mbele lazima wajue ndio ugumu wa mashindano unavyoongezeka, hivyo benchi la ufundi linatakiwa kukaa na wachezaji ili kuwaeleza nini kilichopo mbele yao"

“Ni vema Simba wakaenda kucheza mechi hiyo kwa tahadhari kubwa kwani Nkana ni timu nzuri kuliko hata Mbabane, wana uzoefu wa mashindano na wamekuwa wakifanya vema katika mechi nyingi za kimataifa"

Simba itakuwa inasaka ushindi wake wa kwanza dhidi ya Nkana ambayo wamewahi kukutana nayo mara mbili huko nyuma.

Hata hivyo awamu hii Simba imeonekana kuwa na kikosi imara ambacho kinao uwezo wa kuwaondosha Wazambia hao na kutinga hatua ya makundi
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →