Ratiba ya michezo ya ligi kuu ya Tanzania Bara kwa kikosi cha Simba imesimama kutokana na timu hiyo kukabiliwa na michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
Simba tayari ina michezo mitatu ya kiporo na huenda michezo hiyo ikaongezeka kwani wiki ijayo mabingwa hao watetezi wanakabiliwa na mchezo dhidi ya Nkana Fc
Simba inatarajiwa kusafiri katikati ya wiki ijayo kwenda nchini Zambia kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa utakaopigwa Disemba 14.
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema hana wasiwasi na mechi hizo za viporo lakini kwa sasa kipaumbele chake ni katika michuano ya Kimataifa
"Kwa sasa sifikirii ligi, timu yetu inakabiliwa na michezo ya ligi ya mabingwa, tunahitaji kufuzu kwa hatua ya makundi," amesema
"Hatuna wasiwasi na michezo ya kiporo sababu tuna kikosi imara ambacho kitaweza kupata matokeo na kuzifikia timu zilizo mbele yetu"
Ligi Kuu ya Tanzania Bara inaingia mzunguuko wa 16 wikiendi hii, ambapo michezo miwili inatarajiwa kupigwa leo.
Yanga inaongoza ligi hiyo ikiwa na alama 38 ikifuatiwa na Azam Fc yenye alama 36
Yanga na Azam Fc zimeshuka dimbani mara 14 kila moja wakati Simba iliyoshuka dimbani mara 12 inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 27

ADVERTISE HERE