Aussems tayari ameiandaa dozi ya Nkana Fc

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Dec 2018
Aussems tayari ameiandaa dozi ya Nkana Fc
Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems amewaambia mashabiki na wanachama wa klabu hiyo wasiwe na wasiwasi kabisa juu ya Nkana ya Zambia watakayokutana nayo katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Aussems ambaye kikosi chake kimefuzu hatua ya awali ya mashindano hayo na sasa watacheza na Nkana mechi ya raundi ya kwanza na mchezo wa kwanza utapigwa nchini Zambia Desemba 14 na wa marudiano utakuwa Desemba 21 jijini Dar es salaam

Amesema, watatumia kipindi cha wiki moja kufanya maandalizi juu ya mchezo huo na kwa sababu ameshajua wapinzani wao ni wa aina gani haiwasumbui.

"Tunakwenda kujiandaa kwa ajili ya mchezo huo na kikubwa ni kwamba tuna timu nzuri ya kucheza mashindano hayo kwa nguvu na kufanya vizuri bila wasiwasi,"alisema Aussems aliyesisitiza kwa sasa kikosi chake hakina majeruhi hata mmoja.

Amesema, haina ubishi kama ilivyotokea Eswatini na kwa timu hiyo ya Zambia itakuwa hivyo:

"Nilianza kuzifuatilia zamani hizo timu ambazo tulitarajia kukutana nazo hivyo Nkana pia ilikuwa miongoni mwao kilichobaki ni kazi tu."

Akizungumzia kwa namna gani alivyopokea kuanza mechi yao ugenini na ya marudiano nyumbani: "Kwetu ni vizuri ingawa ni mpango wa ratiba ilivyo, tulianza kucheza nyumbani na Mbabane na sasa tunaanzia ugenini kwa Nkana."

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’