Wakatijina la kiungo wa kimataifa wa Simba Mzambia, Clatous Chama likiwa ndio habari ya mjini, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime, amesema mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, "wamelamba dume" kwa mchezaji huyo.
Chama alifunga mabao mawili katika ushindi wa 4-0 katika mechi ya marudiano dhidi ya Mbabane Swallows iliyochezwa juzi na akifunga bao wiki iliyopita wakati Simba ikipata ushindi wa mabao 4-1 nyumbani.
Maxime amesema Chama ana kiwango bora na ndiyo maana 'halisi' ya mchezaji wa kimataifa anavyotakiwa.
Maxime amesema nyota huyo ambaye anaichezea pia timu ya Taifa ya Zambia (Chipolopolo), anaisaidia klabu yake kufanya vizuri na vile vile anawafanya wachezaji wengine kujituma ili kuonyesha uwezo wao unaotakiwa.
"Chama ni mashine, ana uwezo na anajua nini anachofanya, anaoneysha vitu vyake uwanjani," Mexime amenukuliwa na gazeti la Nipashe
Baada ya kuitoa Mbabane Swallows, Simba sasa imetinga raundi ya kwanza ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na itacheza na Nkana FC ya Zambia
Mchezo wa kwanza utapigwa nchini Zambia kati ya Disemba 18-19 na mchezo wa marudiano kupigwa uwanja wa Taifa wiki moja baadae

ADVERTISE HERE