Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara hakusita kumwagia sifa kiungo fundi wa klabu hiyo Cleotus Chama 'Mwamba wa Lusaka' baada ya hapo jana kuisaidia Simba kuifumua Mbabane Swallows mabao 4-0 na kutinga raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa kwa ushindi wa jumla wa mabao 8-1
Chama alifunga mabao mawili kwenye mchezo huo huku pia akiwa amefunga bao moja kwenye mchezo wa kwanza.
Manara anaamini Chama ana uwezo mkubwa ambao pengine anaweza kucheza katika timu yoyote duniani.
"Hivi Barcelona kwa nini wanajifanyia roho mbaya wenyewe? Pengo la Iniesta duniani litazibwa na Clatous Chama tu!!," ameandika Manara kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.
"Anaufanya mchezo wa mpira uwe rahisi sana,ni kama kusukuma mdomoni tonge la Ugali kwa Mlenda!Chama ni bora kuliko kiungo yoyote kuwahi kucheza Tanzania kando ya Sunday Manara!
"Ni bora kama Luca Modric. Mpira hauhitaji hadi mpigane vichwa na kutoana ngeu, ni rahisi tu"
Tangu atue Simba mwanzoni mwa msimu huu Chama amekuwa katika kiwango bora sana akiisaidia timu hiyo kupata matokeo katika michezo mingi anayokuwa dimbani
Aina yake ya uchezaji imewateka wadau wengi wa soka na hakuna ubishi Chama ndiye kiungo bora kabisa kwa wakati huu hapa Tanzania

ADVERTISE HERE