Kwa Simba hii, yajayo yanafurahisha ligi ya mabingwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 Dec 2018
Kwa Simba hii, yajayo yanafurahisha ligi ya mabingwa
Msimu huu Simba inaweza kurudia kile ilichofanya mwaka 1993 kwa kutinga fainali ya michuano ya kombe la Washindi (Sasa klabu bingwa) kutokana na uimara wa kikosi chake.

Baada ya kuiondosha Mbabane Swallows kwa ushindi wa jumla ya mabao 8-1, njia ni nyeupe kwa Simba kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa sasa ikibaki na michezo miwili tu kabla ya kutinga hatua hiyo.

Kocha Patrick Aussems ametengeneza timu imara inayocheza kandanda safi na la kuvutia. Kikosi hiki cha Aussems kinaweza kufanya mambo makubwa sana msimu huu.

Aidha Bilionea Mohammed Dewji 'MO' mwekezaji wa klabu ya Simba anastahili pongezi kwa uthubutu wake kwani uwekezaji aliofanya umetengeneza kikosi hiki cha maangamizi ambacho dalili zinaonyesha kuleta mambo makubwa huko mbeleni

Mbabane Swallows haikuwa timu ya kubeza, msimu uliopita ilitinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa.

Kipigo walichopata kinaakisi uimara wa kikosi cha Simba na sio kwamba timu hiyo ni dhaifu.

Kazi iliyobaki kwa Aussems na vijana wake ni kuhakikisha wanakamilisha hatua iliyobaki kwa kushinda michezo ya raundi ya kwanza ili kutinga hatua ya makundi.

Katika hatua hiyo kwa Simba hii lolote linaweza kutokea!
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
10m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’