Nahodha wa Simba John Bocco amesema wameufahamu udhaifu wa wapinzani wao na hivyo hawahofii kuwakabili leo kwenye mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa barani Afrika
Bocco alipachika mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 4-1 iliyopata Simba dhidi ya Mbabane Swallows wiki iliyopita
"Mchezo wa kwanza ulitusaidia kuwafahamu vizuri wapinzani wetu," amesema Bocco
"Tunajua mchezo wa leo hautakuwa mwepesi kwa kuwa nao watakuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani lakini tutahakikisha tunapata matokeo yatakayotuwezesha kusonga mbele hatua inayofuata"
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na lengo la kuibuka na ushindi bila ya kujali ushindi mnono waliopata nyumbani
Matokeo ya sare, ushindi au hata kufungwa chini ya mabao mawili, yatatosha kuivusha Simba kutinga raundi ya kwanza

ADVERTISE HERE