Kikosi cha Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo kimefanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Mavuso utakaotumika kesho katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Mbabane Swallows.
Mchezo huo wa marudiano unatarajiwa kuanza saa kumi na nusu jioni kwa saa za Tanzania
Mabingwa hao wa nchi wako Eswatini tangu jana wakiwa na ari kubwa ya kupata matokeo kwenye mchezo huo ili waweze kutinga raundi ya kwanza
Kocha Mkuu wa timu hiyo Patrick Aussems amesema wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na lengo la kushinda bila ya kujali ushindi mnono waliopata kwenye mchezo wa kwanza.
Simba inahitaji ushindi, sare au hata ikifungwa chini ya mabao matatu inaweza kusonga mbele raundi ya kwanza kufuatia ushindi wa mabao 4-1 iliyopata kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa wiki iliyopita

ADVERTISE HERE