Mlinda lango namba mbili wa timu ya Taifa Beno Kakolanya inaelezwa amevunja mkataba wake katika klabu ya Yanga baada ya timu hiyo kushindwa kumlipa kwa miezi mitano.
Taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii jana zimebainisha kuwa Kakolanya tayari ameandika barua TFF akibainisha uamuzi wake huo baada ya Yanga kushindwa kutimiza masharti ya mkataba
Wakati hayo yakiendelea, inaelezwa kuwa mabosi wa usajili wa Simba wanaangalia uwezekano wa kumsajili mlinda lango huyo ili kumpa changamoto Aishi Manula.
Simba inaangalia uwezekano wa kusajili mlinda lango mwingine baada ya Deogratius Munishi 'Dida' aliyesajiliwa mwanzoni mwa msimu kushindwa kufikia ubora uliotarajiwa
Kakolanya alijizolea sifa kwenye mchezo wa kwanza wa watani wa jadi msimu huu akifanikiwa kuinusuru Yanga isitoke na kipigo cha 'mbwa koko' uwanja wa Taifa
Mlinda lango huyo ameruhusu mabao mawili pekee msimu huu katika michezo aliyocheza hivyo kumfanya awe mchezaji sahihi wa kuweza kuchuana na Manula ambaye msimu huu amekuwa akilaumiwa kwa kuruhusu mabao mepesi.

ADVERTISE HERE