Niyonzima aitahadharisha Prisons

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
17 Nov 2017
Niyonzima aitahadharisha Prisons
Kiungo fundi wa Simba Haruna Niyonzima amesema kikosi cha timu hiyo hakijaenda mkoani Mbeya kufanya utalii, bali kimeenda kuchukua alama zote sita kutoka timu za mkoani humo.

Simba tayari imeshachukua alama tatu mkoani Mbeya kwa kuilaza Mbeya City bao 1-0.

Kesho itashuka kwenye dimba la Sokoine kuumana na timu nyingine ya mkoa wa Mbeya, Tanzania Prisons.

Niyonzima amesema kwa maandalizi waliyofanya haoni kama Prisons itaweza kuwazuia wasiondoke na ushindi mkoani Mbeya kesho.

Simba inahitaji kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo ili ijikite kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom.

Kwa sasa Simba ndiyo kinara wa ligi hiyo baada ya kujikusanyia alama 19 kutoka michezo 9 ikiwa sawa na Azam FC, Simba ikiongoza kwa kuwa na utajiri wa mabao.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’