Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wameondoka leo kwenda Eswatini kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa dhidi ya Mbabane Swallows.
Mchezo huo utapigwa Jumatano ijayo, Disemba 05.
Simba tayari iko mbele kwa mabao 4-1 kufuatia ushindi iliyopata dimba la Taifa mapema wiki hii.
Mabingwa hao wa nchi wana kazi ya kulinda ushindi wao huo au pengine hata kuibuka na ushindi ugenini kwani uwezo huo wanao.
Lakini jambo la msingi ni kupata matokeo ambayo yataiwezesha Simba kufuzu kwenda raundi ya kwanza.
Simba inatakiwa kushinda, kutoka sare au hata kufungwa lakini sio zaidi ya mabao mawili.
Habari njema kwa Simba ni kwamba kama itafanikiwa kutinga raundi ya kwanza, basi itakuwa karibu zaidi na tiketi ya kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Kuna uwezekano mkubwa Simba itachuana na Nkana Fc ya Zambia kwenye mchezo wa raundi ya kwanza. Nkana ilishinda mchezo wake wa kwanza licha ya kuwa ugenini nchini Msumbiji.
Nkana sio timu ya kutisha kama ilivyo Mbabane Swallows iliyokula bao 4-1 mbele ya mabingwa hao wa nchi.
Na hata kama ikishindwa kufuzu hatua ya makundi baada ya kutinga raundi ya kwanza, itahamishiwa kwenye michuano ya kombe la Shirikisho ambapo nako itakuwa na nafasi nyingine ya kutinga hatua ya makundi.
Hivyo mchezo dhidi ya Mbabane Swallows una umuhimu wa kipekee kwa Simba.

ADVERTISE HERE