Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kinaondoka kesho Jumapili Dec 02 kuelekea Eswatini kuifuata Mbabane Swallows kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa barani Afrika.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na uongozi wa Simba mapema leo, timu itaondoka saa 12 asubuhi kuelekea nchini Afrika Kusini.
Simba itaunganisha kwenda Eswatini kwa usafiri wa ndege ikitokea Afrika Kusini
Msafara wa Simba utakuwa na wachezaji 20 na viongozi 10 wakiwemo wa benchi la ufundi.
Simba inakwenda Eswatini ikiwa mbele kwa mabao 4-1, ushindi iliyopata kwenye dimba la Taifa mapema wiki hii.
Mabingwa hao wa Tanzania wana nafasi nzuri ya kutinga raundi ya kwanza ikihitaji ushindi, sare au hata ikifungwa chini ya mabao matatu ugenini itafuzu

ADVERTISE HERE