Bocco awatahadharisha wachezaji Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Dec 2018
Bocco awatahadharisha wachezaji Simba
Nahodha wa Simba, John Bocco, amesema hawapaswi kubweteka kwa ushindi waliopata kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mbabane Swallows kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Simba katika mchezo huo ilifanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 na hivyo kujiweka katika mazingira mazuri yakufuzu kwa hatua inayofuata ya michuano hiyo.

Bocco ameliambia gazeti la Nipashe kuwa kwa sasa ni kama wamecheza dakika 45 za kwanza na dakika 45 za pili watazicheza ugenini hivyo ni lazima wajipange kumaliza mchezo huo.

β€œkazi bado haijaisha, tunatakiwa kujipanga na kuweka akilini kuwa bado tuna kazi nzito mbele yetu, tunaenda kucheza ugenini na wenzetu watakuwa wamejipanga kujaribu kubadilisha matokeo,” alisema Bocco.

Aidha, alisema ili kusonga mbele wanapaswa kuwa na nidhamu ya mpira kwa dakika zote 90 watakazocheza ugenini.

β€œKikubwa tutafuata maelekezo ya makocha wetu, na tutajitahidi kupambana kwa nguvu kuweza kusonga mbele,” alisema.

Kikosi cha Simba kinatarajia kuondoka nchini Kesho kwenda Eswatini (zamani ikijulikana kama Swaziland) tayari kwa mchezo huo.

Simba inahitaji sare au ushindi kuweza kusonga mbele na kama itapoteza mchezo huo isipoteze kwa zaidi ya mabao 2-0.

Nipashe
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
34m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’