Simba kuifuata Mbabane Swallows Jumapili

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
30 Nov 2018
Simba kuifuata Mbabane Swallows Jumapili
Kikosi cha mabingwa wa Tanzania Bara Simba kinatarajiwa kuondoka keshokutwa Jumapili Disemba 02 2018 kuelekea Eswatini kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa Barani Afrika.

Mchezo huo utapigwa Jumatano ijayo huko Eswatini (zamani Swaziland)

Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema Simba inatondoka na msafara wa watu 30 utakaojumuisha wachezaji 21 na viongozi tisa wa benchi la ufundi.

Manara amesema Simba itaondoka Jumapili Alfajiri kwa usafiri wa shirika la Ndege la Afrika Kusini hadi nchini humo ambapo itatumia usafiri wa basi kwenda Eswatini.

Msemaji huyo wa mabingwa wa nchi amewaalika mashabiki wa klabu hiyo wanaotaka kusafiri na timu kuchangia kiasi cha dola 300 kwa safari ya kutoka Tanzania hadi Afrika Kusini na dola 50 kwa safari ya kutoka Afrika Kusini hadi Eswatini
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’