Aussems aandaa mkakati wa kuimaliza Mbabane Swallows kwao

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
30 Nov 2018
Aussems aandaa mkakati wa kuimaliza Mbabane Swallows kwao
Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki hii kwenda Eswatini kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa dhidi ya Mbabane Swallows.

Mchezo huo utapigwa Jumatano ijayo huko Swaziland Simba ikiwa mbele kwa mabao 4-1 kufuatia ushindi iliyopata uwanja wa taifa juzi.

Kocha Mkuu wa timu hiyo Patrick Aussems ameendelea na maandalizi ya kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuwa mgumu.

Aussems amesema anakiandaa kikosi chake kuweza kupambana na mazingira watakayokutana nayo ugenini ili kuweza kulinda ushindi na hata kushinda ugenini.

"Ushindi tuliopata hapa nyumbani umetuweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele. Lakini bado tunapaswa kuamini kazi bado hatujaimaliza," amesema Aussems

"Tunakwenda ugenini tukiwa na faida ya mabao matatu, tunajiandaa kikamilifu kuhakikisha tunapata matokeo ugenini yatakayo-tuhakikishia kufuzu hatua inayofuata"

Matokeo ya sare, ushindi au hata kufungwa chini ya mabao matatu yataiwezesha Simba kuitinga raundi ya kwanza ambapo itachuana na mshindi kati ya Nkana Fc dhidi ya UD Songo.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
38m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
18h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’