Aussems awapongeza wachezaji Simba kwa ushindi mnono

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Nov 2018
Aussems awapongeza wachezaji Simba kwa ushindi mnono
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amewapongeza wachezaji wa timu hiyo baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Mbabane Swallows kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa hatua ya awali uliopigwa jana katika dimba la Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya mchezo, Aussems alisema waliingia katika mchezo huo wakiwa na lengo la kufunga mabao mengi na bao la mapema liliwasaidia kutimiza malengo yao

Hata hivyo Aussems amesema anatambua mchezo huo bado haujamalizika kwa kuwa kuna dakika nyingine 90 zitakazopigwa ugenini huko Eswatini

"Tumecheza vizuri na nawapongeza vijana wangu kwa kufanikisha ushindi huu. Kile tulichopanga kukifanya tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa," amesema Aussems

"Wapinzani wetu hawakuwa wabaya sana kwani licha ya sisi kutengeneza nafasi nyingi, wao walikuwa wazuri kwenye mashambulizi ya kushitukiza"

"Tumekamilisha asilimia 50 ya mchezo, sasa tunajiandaa kwa ajili ya kukamilisha asilimia 50 nyingine kwenye mchezo wa ugenini wiki ijayo"
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
34m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’