Mohammed Ibrahim 'Mo' ni mmoja wa wachezaji wenye vipaji cha hali katika kikosi cha Simba kinachonolewa na kocha Joseph Omog.
Msimu huu Mo ambaye ndio kwanza ana miaka 22 amekuwa na nafasi finyu katika kikosi cha kwanza cha kocha Omog.
Usajili wa kiungo Haruna Niyonzima kutoka Yanga na Emanuel Okwi umemfanya kiungo mshambuliaji huyo akose nafasi licha ya uwezo wake mkubwa.
Omog amekuwa akipendelea kuwatumia Okwi, Niyonzima na Kichuya kwenye nafasi za ushambuliaji wa pembeni hivyo kumfanya Mo aliyefanya vizuri msimu uliopita 'asugue bench'.
Kumekuwa na tetesi kuwa mchezaji huyo ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu amechoshwa na hali ya kukosa namba katika kikosi cha Simba na kumfanya akose raha.
Japo mwenyewe hajalizungumza hilo waziwazi lakini watu wake wa karibu wanathibitisha kuwa Mo hana furaha.
Kwani anaamini kwa kipaji alichonacho hakupaswa kukaa nje. Pia mchezaji huyo ana ndoto za kwenda kusakata kabumbu nje ya nchi lakini kutopata kwake nafasi ya kuonekana kunamharibia ndoto zake.
Kumekuwa na taarifa ambazo sio rasmi kuwa Mo anaweza kutimkia Yanga mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu.
Yanga imemuhakikisha namba kwenye kikosi cha kwanza. Kikosi cha Yanga kina mapungufu mengi, wana uhaba wa washambuliaji wa pembeni tangu kuondoka kwa Simon Msuva.
Hivyo viongozi wa Simba wasipuuze tetesi hizo kwani Mo anaweza kweli kusajiliwa na Yanga kama ilivyokuwa kwa Ibrahim Ajib.
Ili kumbakisha Msimbazi, benchi la Ufundi ni vyema likampa nafasi ya kucheza japo hata kipindi kimoja ili aendelee kulinda kiwango chake.
Mo anaweza akasaidiana na Haruna Niyonzima au hata Okwi kwa michezo ya mikoani.
Kama Mo akiachwa aondoke Simba, viongozi watapaswa walaumiwe kwani watakuwa wameacha mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu kama ilivyokuwa kwa Ibrahim Ajib.
Pia ni muhimu kwa viongozi kujenga utamaduni wa kuhuisha mikataba ya wachezaji wake muhimu mapema kabla haijamalizika.
Leo nii inashangaza kuona mchezaji kama Shiza Kichuya hakupewa mkataba mpya hadi sasa ambapo mkataba wake unaelekea ukingoni na kuna taarifa kwamba amegoma kusaini mkataba mpya.
Kichuya atakuwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu na anaweza akajiunga na timu yoyote itakayompendeza kama hatapewa ofa nzuri na Simba.
Mo Ibrahim nae mkataba wake utamalizika mwishoni mwa msimu vivyo hivyo anaweza akajiunga Yanga akiwa mchezaji huru kwa kuwa tu mkataba wake uliachwa hadi ufike mwisho.

ADVERTISE HERE