Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba leo wanashuka kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwakabili Mbabane Swallows katika mchezo wa ligi ya mabingwa Barani Afrika, hatua ya awali.
Kikosi cha Simba kinashuka dimbani kikiwa na hamasa na ari ya kushinda mchezo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele kwenye raundi ya kwanza.
Ni mchezo ambao utatoa taswira kwa Simba katika michuano ya ligi ya mabingwa mwaka huu wekundu hao wa Msimbazi wakiwa na malengo ya kutinga hatua ya makundi.
Simba imekuwa ikijifua katika uwanja wa Boko Veterans.
Aidha kuwasili kwa mshambuliaji Emmanuel Okwi aliyechelewa kutokana na kukabiliwa na majukumu ya timu ya Taifa, kumeimarisha zaidi safu ya ushambuliaji ya mabingwa hao wa nchi.
Wachezaji watatu, Shomari Kapombe, Juuko Murshidi na Asante Kwasi watakosa mchezo huo kutokana na kuwa majeruhi.
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema anatambua mchezo huo hautakuwa rahisi lakini kwa maandalizi aliyofanya, ana matumaini makubwa kwa Simba kupata matokeo mazuri leo
Mbabane Swallows ilitua nchini usiku wa kuamkia jana ambapo jana jioni ilifanya mazoezi kwenye uwanja wa Taifa kwa takribani saa moja.
Mchezo unatarajiwa kuanza saa kumi kamili jioni.
KILA LA KHERI WEKUNDU WA MSIMBAZI...

ADVERTISE HERE