Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kesho Jumatano kinashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Mbabane Swallows katika mchezo wa ligi ya mabingwa hatua ya awali.
Maandalizi ya mchezo huo yamekamilika ambapo ni wachezaji watatu pekee wa Simba ambao wamethibitishwa kuwa watakosa mchezo huo kutokana na majeruhi.
Akizungumza katika Mkutano wa waandishi wa habari kuelekea mchezo huo, kocha wa Makipa Muharami Mohammed amesema wachezaji Shomari Kapombe, Juuko Murushid na Asante Kwasi watakosekana kutokana na kuwa majeruhi.
Muharami amesema Simba imefanya maandalizi ya kutosha na iko tayari kwa ajili ya mchezo huo.
"Tumejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huu. Tunawaheshimu wapinzani japo hatuwajui vizuri lakini kwa maandalizi tuliyofanya nadhani tupo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho," amesema

ADVERTISE HERE