Mkude, Chama wakabidhiwa mikoba kuwadhibiti Mbabane Swallows

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
27 Nov 2018
Mkude, Chama wakabidhiwa mikoba kuwadhibiti Mbabane Swallows
Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wapo ka­tika maandalizi makali kwa ajili ya mechi yake ya Juma­tano ya Mligi ya abingwa Afrika dhidi ya Mbabane Swal­lows kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Kocha Mkuu wa timu hiyo Mbel­giji, Patrick Aussems amewapa kazi maalumu viungo wake wawili, Jo­nas Mkude na Mzambia, Cletus Chama.

Mkude alisema kuwa Aussems amefikia hatua hiyo baada ya kukamilisha uchunguzi wake dhidi ya Mbabane Swallows.Alisema katika uchunguzi huo alibaini kuwa Mbabane wapo vizuri sehemu ya kiungo, ndiyo maana akaamua kuwapatia kazi maalumu.

“Kwa sasa tunaendelea kujifua vilivyo ili tuweze kuwa fiti tayari kwa kuifanya kazi hiyo am­bayo kocha ametupatia, ni matumaini yangu kuwa ha­tutamwan­gusha kocha, tutaifan­ya kama anavyotaka.

“Kazi yenyewe hiyo kwa sasa si­wezi kuisema ila kwa yeyote atakayekuja uwanjani siku hiyo ataiona,” alisema Mkude ambaye hucheza nafasi ya kiungo mkabaji akishirikiana vilivyo na Mghana, James Kotei.

Kwa upande wake Cha­ma yeye hucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji anaye­tokea pembeni sawa na Shiza Kichuya.

Mbabane Swallows inayonolewa na kocha wa zamani wa Mbeya City Kinnah Phiri tayari imesili nchini usiku wa kuamkia leo.

GPL
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →