Michuano ya Chalenji kuanza Disemba 03

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Nov 2017
Michuano ya Chalenji kuanza Disemba 03
Shirikisho la soka Afrika ya Mashariki na Kati (CECAFA) limerejesha michuano ya Chalenji ambayo mwaka huu itafanyika nchini Kenya kuanzia Disemba 03, 2017.

Michuano hiyo itashirikisha jumla ya mataifa 10, Libya na Zimbabwe yakiwa miongoni mwa mataifa yaliyoalikwa kwenye michuano hiyo.

Makundi

A
Kenya
Libya
Rwanda
Tanzania
Zanzibar

B
Uganda
Zimbabwe
Burundi
Ethiopia
Sudani Kusini

Bingwa wa michuano hiyo ataondoka na kitita cha Dola elfu 30 huku mshindi wa pili akipata Dola Elfu 20.

Kila timu itacheza michezo minne ambapo timu mbili kutoka kila kundi zitatinga nusu fainali.

Ratiba iliyotolewa na CECAFA leo inaonyesha Kilimanjaro Stars watakuwa wenyeji wa Libya katika mchezo wa ufunguzi Disemba 03 wakifuatiwa mchezo mwingine kati ya Kenya na Rwanda katika mashindano hayo yatayofika tamati Disemba 17.

Kili Stars itawavaa Zanzibar Desemba 7, siku ya sherehe ya Uhuru wa Tanzania Bara Desemba 9, kikosi cha kocha Salum Mayanga kitakuwa na kazi dhidi ya Rwanda na watamaliza mechi ya mwisho dhidi ya Kenya Desemba 11.

Mechi za kundi B zitaanza Desemba 4 kwa Burundi kuikabili Ethiopia wakati Uganda itaonyeshana kazi na Zimbabwe.

Aidha michuano hiyo ya Chalenji itaathiri ratiba ya ligi kuu ya Vodacom ambayo italazimika kusimama kwa wiki mili.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’