Wachezaji wa Kimataifa wa Simba Emmanuel Okwi na Juuko Murshidi wanatarajiwa kuwasili leo kujiunga na kambi ya kikosi cha Simba kinachojiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Mbababe Swallows utakaopigwa keshokutwa Jumatano.
Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema wachezaji hao wamechelewa kurudi kwa kuwa walikuwa na majukumu ya timu ya Taifa ya Uganda.
"Okwi na Juuko walikuwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda kilichokuwa nchini Nigeria kwa ajili ya mchezo wa kirafiki," amesema.
"Uganda ilikwenda Nigeria baada ya mchezo wao dhidi ya Cape Verde"
"Tayari wamepewa ruhusa na leo watawasili kisha kuelekea kambini moja kwa moja kuungana na wachezaji wengine," amesema Manara

ADVERTISE HERE