Beki wa Kimataifa wa Simba Shomari Kapombe ameanza matibabu ya jeraha alilopata wakati akiitumikia timu ya Taifa iliyokuwa ikijiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho.
Kapombe anayetibiwa katika jiji la Cape Town nchini Afrika Kusini amefanyiwa upasuaji leo.

Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Simba, Haji Manara amesema leo itatolewa taarifa rasmi juu ya muda ambao Kapombe anatarajiwa kuwa nje.
"Beki wetu wa Kimataifa, Shomari Kapombe amefanyiwa upasuaji kule Cape Town nchini Afrika Kusini," amesema Manara kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari
"Tunatarajia leo madaktari wanaomtibu watatoa taarifa rasmi ya kitabibu ambayo itabainisha muda ambao Kapombe atakuwa nje."

ADVERTISE HERE