Okwi, Kagere, Bocco wapewa somo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
26 Nov 2018
Okwi, Kagere, Bocco wapewa somo
Manahodha wa zamani wa Simba, Mussa Hassan ‘Mgosi’ na Nassor Masoud ‘Chollo’, wametoa angalizo kwa mastaa wa timu hiyo kuelekea mchezo wao dhidi ya Mbabane Swallow utakaopigwa keshokutwa Jumatano.

Wamesema kwa sasa Simba inahitaji kuvunja rekodi ya kufika mbali na siyo kiki za mchezaji mmoja mmoja ambazo zinaweza kusababisha uchoyo na ubinafsi, jambo ambalo halitakuwa na manufaa kwa timu.

Mgosi, ambaye kwa sasa ni Kocha wa Simba B, aliwataka mastraika wa timu hiyo, John Bocco, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi, kutuliza akili zao akisema mashabiki wanataka matokeo mazuri uwanjani na sio ukubwa wa majina.

Alimchambua Bocco na Kagere walichokifanya kwenye mechi dhidi ya Lipuli, akisema utulivu hafifu ndio chanzo cha kudondosha pointi mbili baada ya kuambulia sare.

“Okwi, Kagere na Bocco ni washambuliaji wenye uwezo wa hali ya juu, wanaweza kubadili matokeo muda wowote ila katika mechi dhidi ya Lipuli walikamia sana na hilo ni tatizo.

"Kama mtu huwezi kufanga basi toa pasi kwa aliyekuwa kwenye nafasi nzuri.

“Simba ya sasa inahitaji matokeo mazuri sio ukubwa wa majina uwanjani, mashabiki na wanachama wanatamani kuona rekodi za kimataifa zinavunjwa,” alisema.

Naye Chollo alisema anakiamini kikosi cha Simba kina wachezaji wenye uzoefu, lakini wanahitaji umakini zaidi na kuweka uzalendo mbele.

"Kuna mambo matatu hapa umakini, kujitambua na uzalendo, basi naamini Simba itafika mbali kimataifa na kuweka rekodi zake,” alisema.

Katika hatua nyingine nahodha wa Simba Bocco amewataka mashabiki kuachana na matokeo ya Lipuli na kugeukia mechi hiyo ya kimataifa ili kupata ushindi.

“Tunahitaji kuyajenga yajayo na kuachana na matokeo yaliopita, ili kufanya vitu vya tofauti katika michuano ya CAF, tuna nafasi ya kufika mbali,” alisema.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
15h ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE →