Moja ya malengo ya klabu ya Simba msimu huu ni angalau kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa inayoanza keshokutwa Jumatano kwa mabingwa hao wa Tanzania Bara kuchuana na Mbabane Swallows.
Mchezo huo wa hatua ya awali utapigwa kwenye uwanja wa Taifa.
Ili kuhakikisha Simba inafanya vizuri, Mwekezaji wa klabu hiyo Mohammed Dewji 'MO' ameahidi kuongeza posho za wachezaji.
Simba imekuwa na kawaida ya kuwatuza wachezaji kila inaposhinda mchezo kwa kuwapa posho kati Tsh 100,000 na 300,000 lakini MO amekusudia kuongeza dau hilo ili kuwaongezea wachezaji mzuka kuelekea mchezo huo
Simba inajifua kwenye uwanja wa Boko Veterans kujiandaa na mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa mabingwa hao wa Tanzania Bara waliorejea rasmi kwenye michuano ya Kimataifa msimu uliopita.
Msimu uliopita Simba ilishiriki michuano ya kombe la Shirikisho na ilifanikiwa kutinga raundi ya kwanza kabla ya kutolewa na Al Masry.
Simba ina rekodi ya kipekee kwenye michuano ya vilabu barani Afrika. Mwaka 1993 Simba ilitinga fainali ya kombe la Washindi (Sasa kombe la shirikisho) barani Afrika

ADVERTISE HERE