Mbabane Swallows haijulikani ilipo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Nov 2018
Mbabane Swallows haijulikani ilipo
Wakati mchezo wa ligi ya mabingwa hatua ya awali kati ya mabingwa wa Tanzania Simba dhidi ya Mbabane Swallows kutoka Eswatini ukitarajiwa kupigwa keshokutwa Jumatano kwenye uwanja wa Taifa, Mbabane haijatoa taarifa yoyote juu ya ujio wao.

Kuna taarifa kuwa timu hiyo huenda tayari imewasili nchini kimyakimya.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, amesema kuwa maandalizi ya mchezo huo yako katika hatua za mwisho na wanawaomba mashabiki, wanachama wa klabu hiyo pamoja na wadau wa soka kujitokeza kuishangilia timu yao.

"Tunaendelea vizuri na maandalizi, malengo yetu ni kupata matokeo mazuri hapa nyumbani ili mechi ya marudiano iwe nyepesi, tumepanga mchezo utaanza saa 10:00 jioni, kiingilio cha chini ni Sh. 5,000, cha juu upande wa VIP A ni Sh. 20,000.

"Lakini mpaka muda huu (jana mchana) bado Mbabane hawajatuma taarifa rasmi za ujio wao," alisema Manara.

Uongozi wa klabu ya Simba baadae leo utazungumza na waandishi wa habari kuelezea maandalizi ya mchezo huo.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’