Wakala wa Salamba afunguka safari ya mchezaji huyo Ulaya

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
25 Nov 2018
Wakala wa Salamba afunguka safari ya mchezaji huyo Ulaya
Wakala wa mshambuliaji wa Simba Adam Salamba amesema kuna timu tatu kutoka barani Ulaya ambazo zimeonyesha nia ya kutaka kumsaini mchezaji huyo.

Jamal Kisongo amesema timu hizo tayari zimepewa taarifa na takwimu za mchezaji huyo kwa ajili ya kwenda kuzifanyia kazi.

Jana Kisongo aliliambia gazeti na Championi kuwa hadi sasa kuna timu tatu zimeleta ofa ya kumtaka Salamba ambapo zimehitaji takwimu zake kujua amecheza mechi ngapi msimu huu na ule uliopita na tayari wamefanya hivyo na kila kitu kinaweza kukamilika Desemba, mwaka huu.

β€œKuna timu tatu ambazo zimeleta ofa za kumtaka Salamba moja kwa moja wakihitaji aende kufanya majaribio ambapo kwanza walihitaji takwimu zake kujua amecheza mechi ngapi msimu uliopita na msimu huu na idadi ya mabao aliyofunga, tayari tumeshakamilisha zoezi hilo kwa kuwasilisha video zake zote alizocheza.

β€œKila kitu kimeshakamilika kwa upande wake lakini tunasubiri muda ufike ndio tujue anaende wapi, kwa sasa ni mapema mno kutaja timu hizo hadi mipango itakapokamilika ila nimeshaongea na mchezaji juu ya kujiandaa na safari,” alisema Kisongo.

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems aliwahi kumtabiria mshambuliaji huyo kuwa huenda akapata nafasi ya kwenda kucheza soka Ulaya kama ataendelea kujituma zaidi kuimarisha kiwango chake kutokana na umri wake kuwa mdogo
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’